Usikate tamaa, Safari bado ni ndefu.


Nimekutana na rafiki zangu wa kidato cha nne, tumeongea mengi ya utotoni na kukumbuka malengo tuliyokuwa tukijiwekea aidha kwa mzaha ama kwa kudhamiria, ila hiyo haina sana mashiko kwa sasa maana, wengi wetu tumefanikia kupata maisha ya wastani na bado tunaendelea kutafuta ndoto zetu.

Kwa kipindi cha masomo shuleni, hatukuweza kujua wapi tutafika, na ni nini tutafanya. Kwa sababu ilikuwa shule ya wamisionari, kwa hiyo ilikuwa rahisi sana kujua labda unaweza kwenda kusomea upadri. Ilikuwa ni kitu chenye mwelekeo usio sahihi kwa wakati ule maana wito pekee ndio ungeweza kuhakiki dhumuni lako la kuwa Padri.

Kwa maana hiyo wengi wetu tulimaliza na kufaulu vizuri na kuendelea na masomo na wengine walishindwa kutokana na hali ngumu ya uchumi katika familia na wengine mpaka leo sijui wapo wapi, ila naamini bado wanaendelea na mapambano ya maisha.

Mimi mwenyewe, nilikuwa na malengo mbali mbali katika maisha, na kuhakikisha ninapata maisha bora (japo ilikuwa ngumu sana kujua maisha bora ni yapi kwa wakati ule).

Katika safari yote niliyopitia na labda wengi wenu mnaosoma maandishi haya leo hii mtakuwa mmepitia pia. Yapo mambo ambayo katika maisha, yanaweza kukuvunja moyo na kukata tamaa ya maisha. tumesikia watu mbalimbali wanachukua uhai wao wenyewe, sio kwa sababu wanapenda ila kwa sababu ya kitu fulani ambacho kimewaharibia mwenendo wa maisha. Itabidi tukubali kwamba tumejaliwa utofauti katika kutafuta mustakabali wa mambo mbali mbali, katika kuchambua na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha japo kupitia kipindi kigumu.

Maisha sio lele mama, inabidi tufunge mkanda, tuwe na uvumilivu na kujua mwelekeo wa maisha utakaokufaa. Usisubiri kuambiwa kwamba njia hii unayotumia sio sahihi ama hii ni sahihi.

Wewe pekee ndio mwamuzi wa mwisho wa maamuzi utakayofanya juu ya maisha yako. Jua ni kitu gani unataka na ukifanyie kazi kwa bidii maana bila kufanya hivyo hatuwezi kamwe kupata majibu ya maisha yetu na ya baadae.

Hivyo kukata tamaa si jambo la kufikiria kabisa, maisha yapo yanatusubiri kwa hali  na mali.

Jiwekee malengo, kuwa na uvumilivu, acha kufanya mambo yasiyo na umuhimu, fanya uchambuzi wa mambo kabla ya kutenda, tenda kwa uaminifu; ukifanikiwa kukamilisha mambo haya machache, maisha hayatokuwa magumu sana naamini.

 

Mwandishi: Felix Massinda

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s